• HABARI MPYA

    Tuesday, April 15, 2014

    YANGA SC WAPIGA ‘NDONDO’ MOSHI

    Na Renatus Mahima, Arusha
    KIKOSI cha Yanga kimelazimika kupiga kambi ya siku mbili mjini Moshi ili kicheze mechi ya 'ndondo' kabla ya kuikabili Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi.
    Boniface Mkwasa, kocha msaidizi wa Yanga, ameithibitishia BIN ZUBEIRY jana mchana kwamba timu yao iliyoondoka jijini hapa jana asubuhi imeweka kambi ya muda mjini Moshi, Kilimanjaro na kesho jioni itacheza mechi ya kirafiki na moja ya timu za mjini humo.
    Kutoka Ligi ya Mabingwa hadi ndondo; Mchezaji wa Yanga, Mrisho Ngassa akiwania mpira dhidi ya mchezaji wa Al Ahly ya Misri katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu. Yanga ilitolewa na timu hiyo ya Cairo. 

    "Leo (jana) tunalala Moshi kwa sababu kesho (leo) tutacheza mechi ya kirafiki kabla ya kuendelea na safari ya kurejea Dar es Salaam," amesema Mkwasa.
    Kutopitika kirahisi kwa daraja la Mto Ruvu, Pwani huenda ndiyo sababu kubwa iliyokikwamisha kikosi hicho cha Wanajangwani kutorejea moja kwa moja Dar es Salaam.
    Pengine pia kutoambulia chochote katika mapato ya mlangoni katika mechi yao ya jana dhidi ya Oljoro JKT nako kunaweza kuwa sababu nyingine kwa sababu Shiorikisho la Soka nchini (TFF) limeshatangaza kuzuia mapato ya milangoni ya Yanga ili kuwalipa wachezaji wao wa zamani Ndlovu na Steben Malashi kufuatia agizo la Mahakama Kuu (Kitengo cha Kazi).
    Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Arusha, Adam Brown, mechi ya jana ya Oljoro dhidi ya Yanga imeingiza Sh. milioni 25 huku timu ikipata mgawo wa Sh. milioni tano.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WAPIGA ‘NDONDO’ MOSHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top