• HABARI MPYA

    Monday, July 21, 2014

    KIFAA KINGINE CHA KIMATAIFA CHATUA KESHO SIMBA SC, WAKALI WATATU WA HAPA HAPA NAO KUTUA MSIMBAZI

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KIUNGO wa kimataifa wa Kenya, Paul Mungai Kiongera anatarajiwa kutua nchini kesho kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kujiunga na klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam. 
    Mchezaji huyo wa KCB ya Ligi Kuu ya nchini, anakuja nchini kwa mazungumzo ya mwisho baada ya mazungumzo ya awali kwa simu na kama yatakwenda vizuri, atasaini Mkataba.
    Aidha, kiungo Mrundi Pierre Kwizera baada ya kufikia makubaliano na uongozi wa Simba SC anarejea Ivory Coast kumalizana na klabu yake, Afad Abidjan ili aje kusaini Mkataba.
    Paul Kiongera atawasili Jumanne Dar es Salaam kuja kukamilisha mipango ya kujiunga na Simba SC

    Simba SC pia ipo kwenye mazungumzo na klabu za JKT Ruvu, Ruvu Shooting na Coastal Union kwa ajili ya kuwanunua wachezaji Edward Charles, Elias Maguri na Abdul Banda.
    BIN ZUBEIRY inafahamu mazungumzo hayo yanaendelea vizuri na kuna uwezekano wachezaji hao wakahamia Msimbazi kwa ajili ya msimu ujao.
    Kwa upande mwingine, Simba SC itakutana na wachezaji wake ambao bado wana mikataba, lakini haiwahitaji kwa sasa ili kujadiliana nao kuvunja kandarasi hizo.
    Hao ni kipa Abuu Hashimu, beki Hassan Khatib, viungo Abulhalim Humud ‘Gaucho’, Ramadhani Chombo ‘Redondo na washambuliaji Betram Mombeki na Christopher Edward.  
    Tayari Simba SC imefikia makubaliano ya kuachana na beki Mrundi, Kaze Gilbert anayetakiwa na klabu yake ya zamani, Vital’O.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIFAA KINGINE CHA KIMATAIFA CHATUA KESHO SIMBA SC, WAKALI WATATU WA HAPA HAPA NAO KUTUA MSIMBAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top