• HABARI MPYA

    Wednesday, September 10, 2014

    BAD NEWS; COUTINHO AUMIA YANGA IKICHEZA NA POLISI LOYOLA LEO, HUENDA AKAIKOSA MECHI YA NGAO NA AZAM JUMAPILI TAIFA

    Na Nagma Khalid, DAR ES SALAAM
    YANGA SC inaweza ikaingia kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii Jumapili dhidi ya Azam FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam bila ya mchezaji wake mahiri, Mbrazil Andrey Coutinho.  
    Hiyo inafuatia kiungo huyo kuumia katika mchezo wa kirafiki asubuhi ya leo dhidi ya Polisi ya Dar es Salaam Uwanja wa sekondari Loyola, Mabibio, Dar es Salaam.
    Coutinho alikuwa anajaribu kugeuka apige mpira, akateguka kifundo cha mguu na kushindwa kuendelea na mchezo uliomalizika kwa sare ya 0-0.
    Pigo Jangwani; Andrey Coutinho ameumia leo akicheza mechi ya kirafiki na Polisi

    Taarifa za awali zinasema mchezaji huyo anatakiwa kuwa nje kati ya wiki mbili hadi tatu, lakini taarifa rasmi juu ya maumivu yake itatolewa na klabu hiyo baada ya kufanyiwa vipimo.
    Coutinho tayari ameziteka nafasi za wapenzi wa Yanga SC kutokana na soka yake nzuri aliyoionyesha katika kipindi kifupi tangu ajiunge na timu hiyo na unaweza kusema ni moja ya wachezaji tegemeo la timu hiyo kwa sasa.
    Pamoja na kuumia kwa Coutinho, habari njema kuelekea mchezo wa Ngao Jumapili ni kwamba, mchezaji anayeongoza kwa mabao katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Mrisho Ngassa ameanza mazoezi leo baada ya awali kuripotiwa kugoma kushinikiza maslahi yake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BAD NEWS; COUTINHO AUMIA YANGA IKICHEZA NA POLISI LOYOLA LEO, HUENDA AKAIKOSA MECHI YA NGAO NA AZAM JUMAPILI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top