• HABARI MPYA

    Wednesday, October 15, 2014

    SIMBA SC YALALA 2-0 KWA JOMO COSMOS

    SIMBA SC imekamilisha mechi zake za kirafiki za kujipima nguvu katika kambi yake ya Afrika kwa kufungwa mabao 2-0 na Jomo Cosmos mjini Johannesburg jioni hii.
    Pamoja na kufungwa na timu hiyo ya Daraja la Kwanza, inayomilikiwa na kufundishwa na gwiji wa soka Afrika Kusini, Jomo ‘Black Prince’ Sono, Simba SC ilicheza soka ya kuvutia.
    Huo ni mchezo wa tatu kwa Simba SC katika kambi yake ya Afrika Kusini tangu iwasili Oktoba 8, mwaka huu kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
    Katika mchezo wake wa kwanza, Simba SC ililazimishwa sare ya bila kufungana na Orlando Pirates kabla ya kufungwa mabao 4-2 na Bidvest Wits, au Wits University.
    Simba SC itaendelea na mazoezi kesho na inatarajiwa kurejea Dar es Salaam Ijumaa tayari kwa mchezo wa Jumamosi, unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YALALA 2-0 KWA JOMO COSMOS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top