• HABARI MPYA

    Friday, November 21, 2014

    ARSENAL NI VIBONDE WA 'KUPIKA NA KUPAKUA' KWA MAN UNITED, MECHI 11 ZILIZOPITA WAMESHNDA MOJA TU

    REKODI YAO YA KWENYE LIGI TANGU 2009

    Mechi walizocheza: 11 
    Man United walizoshinda: 7 
    Arsenal waliyoshinda: 1
    Walizotoka sare: 
    MECHI kati ya Arsenal dhidi ya Manchester United wakati wote imekuwa moja ya michezo ya kusisimua katika historia ya  Ligi Kuu ya England – lakini The Gunners wameshinda mechi moja tu kati ya 11 zilizopita baina ya klabu hizo.
    Louis van Gaal atasafiri na kikosi chake chenye majeruhi kibao hadi Uwanja wa Emirates Jumamosi mchana akitambua kwamba timu yake imekuwa na historia nzuri siku za karibuni dhidi ya wapinzani wake hao.
    Licha ya kuboronga msimu uliopita, lakini bado United ilijimudu kuichapa Arsenal 1-0 Uwanja wa Old Trafford na kutoka nayo sare ya bila kufungana katika mchezo mwingine Kaskazini mwa London.
    Aaron Ramsey scored the only goal of the game the last time Arsenal beat Manchester United in 2011
    Aaron Ramsey alifunga bao pekee mara ya mwisho Arsenal ilipoifunga Manchester United mwaka 2011
    Arsenal beat Manchester United 1-0 in 2011 - their only win in the last 11 games against United
    Arsenal iliifunga Manchester United 1-0 mwaka 2011 - ushindi wao pekee katika mechi 11 dhidi ya United
    Danny Welbeck - who is now at Arsenal - scored the last time Manchester United won at the Emirates in 2012
    Danny Welbeck - ambaye kwa sasa yupo Arsenal - alifunga bao la ushindi dakika ya mwisho Manchester United ikishinda Uwanja wa Emirates mwaka 2012
    Former Arsenal striker Robin van Persie scored the winner for United at Old Trafford last season
    Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Robin van Persie alifunga bao la ushindi kwa United Uwanja wa Old Trafford msimu uliopita

    MECHI BAINA YA ARSENAL NA MAN UTD
    Feb 12, 2014Arsenal0-0Man Utd
    Nov 10, 2013Man Utd1-0Arsenal
    Apr 28, 2013Arsenal1-1Man Utd
    Nov 3, 2012Man Utd  2-1Arsenal
    Jan 22, 2012Arsenal1-2Man Utd
    Ago 28, 2011Man Utd8-2Arsenal
    May 1, 2011Arsenal1-0Man Utd
    Dec 13, 2010Man Utd1-0Arsenal
    Jan 31, 2010Arsenal1-3Man Utd
    Ago 29, 2009Man Utd2-1Arsenal
    May 16, 2009Man Utd0-0Arsenal
    Wakati kocha Sir Alex Ferguson akiwa katika msimu wake wa mwisho Old Trafford, mabao ya Robin van Persie na Patrice Evra yaliipa United ushindi wa 2-1 nyumbani wakati Van Persie pia alifunga tena dhidi ya Arsenal aliporejea Emirates baadaye msimu huo kusawazisha baada ya Theo Walcott kuanza kufunga na kufanya sare ya 1-1.
    Ushindi wa mwisho wa Arsenal katika Ligi Kuu ya England dhidi ya United ulikuwa Mei mwaka 2011 wakati Aaron Ramsey alipofunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 nyumbani.
    Kutoka kwenye kikosi cha Arsenal wakati huo, wachezaji watano bado wapo klabuni, akiwemo kipa Wojciech Szczesny, Laurent Koscielny, Walcott, Ramsey na Jack Wilshere.
    Lakini ikiwa Wenger anatafuta ahueni anahitaji kutazama juu ya rekodi ya ugenini ya United, bado hawajashinda mechi yoyote ugenini msimu huu na hawajachukua pointi tatu katika mechi zao za ugenini tangu Aprili 5, mwaka huu walipoifunga Newcastle 4-0.
    Misimu iliyopita, mechi kati ya Arsenal vs Manchester United ilikuwa ya kuamua bingwa, lakini mwaka huu inaonekana kama ni mechi ya kuwania nafasi ya nne na ya mwisho ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.
    Lakini kikubwa zaidi, The Gunners wanatarajiwa kufuta uteja wao kwa United. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL NI VIBONDE WA 'KUPIKA NA KUPAKUA' KWA MAN UNITED, MECHI 11 ZILIZOPITA WAMESHNDA MOJA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top