• HABARI MPYA

    Thursday, November 20, 2014

    BARAKA KARASHANI KUZIKWA KESHO SINZA MAKABURINI

    "Habari wadau, naomba kuwajulisha kuwa mazishi ya aliyekuwa mwanachama mwenzetu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Baraka Karashani, aliyefariki jana, yatafanyika kesho alasiri katika makaburi ya Sinza, Dar es Salaam. Tunaomba tushirikiane katika kuhifadhi mwili wa mpendwa wetu, ambapo sekreterieti ya TASWA imemteua Majuto Omary ambaye ni Mwenyekiti wa TASWA FC, Mwani Nyangassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Zena Chande Mhazini Msaidizi  kusimamia michango mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari za michezo nchini kwa ajili ya msiba huo. Nawasilisha, Amir Mhando, Katibu Mkuu TASWA, 20/11/2014,".
    Baraka Karashani enzi za uhai wake
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BARAKA KARASHANI KUZIKWA KESHO SINZA MAKABURINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top