• HABARI MPYA

    Sunday, November 16, 2014

    MBEYA CITY NA MWAMBUSI SASA WAPISHANA KAULI

    Na Emanuel Madafa, MBEYA 
    Licha ya Kocha Juma Mwambusi kutangaza rasmi kuondoka kuifundisha  klabu ya Mbeya City, uongozi wa klabu hiyo umemruka kocha huyo na kudai  kuwa bado haujapata barua rasmi ya kujiuzulu kwakwe  au kusitisha mkataba  kwa kocha mkuu huyo.
    Akizungumza kwa  njia ya simu, Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Emmanuel Kimbe, amesema wao kama uongozi bado haujapokea taarifa yoyote kwa njia yamdomo wala barua rasmi ya kujiuzulu kwa kocha huyo.
    Amesema, kiongozi anapojiuzulu kuna taratibu ambazo anapaswa kuzifuata kama kuwasilisha barua hivyo wao hawajapokea barua hiyo bali taarifa za kujiuzulu kwa kocha hizo wamezisikia kwenye vyombo vya habari.
    Naye, Mwenyekiti wa bodi ya klabu ya Mbeya City, Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Athanas Kapunga, amesema taarifa ya kujiuzulu kwa kocha huyo amezisikia kwenye vyombo vya habari na kwamba taarifa rasmi bado hajazipata.

    Akizungumza kwa njia ya simu, Mwambusi alikiri kuwa ni kweli amejiuzulu lakini alipotakiwa kutoa ufafanuzi kwanini amejiuzulu bila ya kutoa taarifa rasmi kwa mwajiri wake ambaye ni Halmashauri ya Jiji la Mbeya, alisita kutoa majibu ya swali hilo.
    “Kweli nimejiuzulu lakini siwezi kuzungumzia suala la kuwasilisha barua kwa mwajiri kwani ni mapena sana na sasa nimechoka kupokea simu za watu naombeni mniache nilale”alisema Mwambusi.
    Habari za uhakika zilizolifikia blog hii  kutoka ndani ya uongozi wa Jiji la Mbeya, ziunaeleza kuwa  halmashauri hiyo chini ya Meya Kapunga tayari ilianza zoezi la kukutana na wadau mbalimba pamoja na wachezaji ili kubaini changamoto zinazoikabili timu hiyo.
    Hata hivyo,taarifa zinaeleza kuwa   katika vikao hivyo kati ya wadau na Meya, lawama nyingi zinadaiwa kuelekezwa kwa kocha huyo pamoja na uongozi mzima wa timu hiyo.
    Moja ya shutumna anazotuhumiwa kocha huyo mbali ya kukosa mbinu mpya za kifundi, pia amekuwa kinara  wa kuwagawa wachezaji kwa kutoa namba kiupendeleo.
    Aidha wadau hao pia wamenena yao kwa kudai kuwa  Mwambusi, ni kocha  mzuri lakini  ameshindwa kuwaunganisha wachezaji kwa kuwaweka pamoja na kwamba kiufundi ukimuongelea kocha huyo ni kwamba hana ripoti nzuri.
    Walisema Mwambusi huwa anafanya vizuri na timu kwa msimu uleule anao kabidhiwa na timu lakini kwa msimu unaofuata huwa afanyi vizuri,”anasema,
    Mfano mpaka sasa Mwambusi ameweza kushusha timu tano daraja zilizokuwa ligi kuu, ukianza na timu ya Palison ya Arusha iliyokuwa ikimilikiwa na askofu Molele, Mwambusi aliiendesha timu hiyo na kufanya vizuri lakini mwaka uliofuata timu hiyo ilishuka daraja.
    Walienda mbali zaidi kwa kudai kuwa alitoka timu hiyo akaenda Moro united ambayo aliiendesha kwa msimu mmoja na uliofuata ilishuka daraja akaenda kuishika Polisi Dodoma  alidumu nayo kwa msimu mmoja msimu uliofuata ilishuka  na huyo huyo Mwambusi ndio aliyeishusha Tukuyu stars mwaka 2008.
    Licha ya kwamba mwaka huo huo aliiwezesha kucheza na kushika nafasi ya nane bora lakini mwaka 2011 alimaliza kwa kuishusha daraja timu ya Tanzania Prisons.
    “Hivyo mambo ya Mbeya City kutofanya vizuri mimi si shangai na hii siongelei uzaindiki nasema ukweli kihistoria Mwambusi anataarifa ya kwamba aliwahi kuwa mchezaji wala mpira haujii hivyo uwezo wa kusajili mchezaji mzuri hana,” anasema.
    Hadi sasa Mbeya City ndio tumu inayoshika mkia katika msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara ikiwa imevuna pointi 5 baada ya kushinda mchezo mmoja, kutoa sare miwili na kupoteza michezo mitatu.
    Mbeya city ambayo msimu wa mwaka jana ilikuwa ni moto wa kuotea mbali na kuzitia mshituko mkubwa klabu kongwe kama Simba na Yanga ikiwemo Azam FC, msimu huu wamekuja kivingine huku wakiwa wamepoteza makali yao ya ushindi popote.
    IMEHAMISHWA KUTOKA; http://www.jamiimoja.blogspot.com
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY NA MWAMBUSI SASA WAPISHANA KAULI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top