• HABARI MPYA

    Sunday, November 16, 2014

    ULIMWENGU AFUNGA, AKOSA PENALTI STARS IKITOA SARE 1-1 NA SWAZILAND SOMHLOLO

    Na Mwandishi Wetu, MBABANE
    TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji Swaziland katika mchezo wa irafiki wa kimataifa uliofanyika uwanja wa Taifa wa Somhlolo mjini Mbabane.
    Katika mchezo huo unaotambuliwa na Shiriksiho la Soka la Kimataifa (FIFA), Swaziland walikuwa wa kwanza kupata bao kipindi cha kwanza, kabla ya Stars kusawazisha kupitia kwa Thomas Ulimwengu kwa kichwa kipindi cha pili akiunganisha krosi ya Erasto Nyoni.
    Ulimwengu aliikosesha Stars bao la pili dakika za mwishoni baada ya kukosa penalti kufuatia mchezaji wa Swaziland kuunawa mpira katika harakati za kuokoa krosi ya Oscar Joshua.
    Thomas Ulimwengu kushoto ameifungia bao Stars sare ya 1-1 na Swaziland, ingawa pia amekosa penalti

    Huo ni mchezo wa 10 Nooij anaiongoza Stars tangu arithi mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen Apili mwaka huu, katika mechi tisa za awali,  alishinda tatu, sare tatu na kufungwa tatu.
    Nooij alianza kwa sare ya 0-0 na Malawi katika mchezo wa kirafiki mjini Mbeya, kabla ya kushinda 
    1-0 dhidi ya Zimbabwe mchezo wa kufuzu AFCON mjini Dar es Salaam.
    Akashinda tena 1-0 na Malawi katika mchezo wa kirafiki Dar es Salaam kabla ya sare ya 2-2 na Zimbabwe kufuzu AFCON mjini Harare na baadaye kufungwa 4-2 na Botswana katika mchezo wa kirafiki mjini Gaborone.
    Akatoa sare ya 2-2 na Msumbiji mjini Dar es Salaam kufuzu kabla ya kwenda kufungwa 2-1 katika mchezo wa marudiano mjini Maputo na kisha kufungwa 2-0 na Burundi mchezo wa kirafiki mjini Bujumbura.
    Mechi iliyopita, Nooij aliiongoza Stars kushinda kwa kishindo, mabao 4-1 dhidi ya Benin, ukiwa pia mchezo wa kirafiki Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Kikosi cha Taifa Stars kilichoanza leo kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Oscar Joshua, Said Mourad, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mwinyi Kazimoto, Thomas Ulimwengu, Juma Luizio/Simon Msuva na Amri Kiemba/Nadir Haroub.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ULIMWENGU AFUNGA, AKOSA PENALTI STARS IKITOA SARE 1-1 NA SWAZILAND SOMHLOLO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top