• HABARI MPYA

    Wednesday, February 25, 2015

    AZAM FC WAPOKEWA ‘KIGAIDI’ SUDAN, WAPEWA ‘GARI LA MKAA’, WACHEZAJI WAPIGISHWA KWATA UWANJA WA NDEGE

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Azam FC wamepata mapokezi ya ‘kigaidi’ mjini Khartoum, Sudan baada ya kuwasili usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya mchezo na wenyeji, El Merreikh.
    Kwanza, walipotua Uwanja wa Ndege, wachezaji na msafara mzima walianza kufanyiwa vitimbi na watu wa Idara ya Uhamiaji katika kupatiwa visa za kuingia nchini humo.
    Baada ya kuufuzu mtihani huo, walikutana na visa zaidi walipotoka nje ya Uwanja wa Ndege, kufokewa na watu waliokwenda kuwapokea, kabla ya kwenda kutaka kuwapakia katika basi bovu na baya aina ya Coaster.
    Hili ndilo basi ambalo El Merreikh wamewapatia Azam FC baada ya kuwasili Khartoum
    Basi hili mwonekano wake kama limetoka vitani
    Basi aina ya Coaster ambalo wamepewa Azam FC Sudan

    Pamoja na hayo, Azam FC kwa kuwa walijua watakutana na hali kama hiyo, hawakuonekana kustaajabu, badala yake kuvumilia yote. Hawakutumia basi hilo, walikodi basi lingine zuri na kwenda katika kambi yao. 
    Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ameiambia BIN ZUBEIRY kwa simu kutoka Khartoum kwamba wamefanyiwa mambo ambayo kwa ujumla si ya kuanamichezo.
    “Tunarekodi kila kitu na tutatuma CAF (Shirikisho la Soka Afrika). Sisi hatuna wasiwasi nao, kwa sababu tunawajua,”amesema. 
    Kikosi cha wachezaji 23 wa Azam kimewasili Khartoum tayari kwa mchezo wa marudiano, Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika mwishoni mwa wiki.
    Azam FC inahitaji hata sare au kutofungwa kwa wastani wa zaidi ya bao 1-0 ili kusoga mbele kwenye michuano hiyo, baada ya awali kushinda 2-0 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam wiki iliyopita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC WAPOKEWA ‘KIGAIDI’ SUDAN, WAPEWA ‘GARI LA MKAA’, WACHEZAJI WAPIGISHWA KWATA UWANJA WA NDEGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top