• HABARI MPYA

    Wednesday, April 15, 2015

    ETOILE WAJA KESHO DAR KWA NDEGE MAALUM

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    WAPINZANI wa Yanga SC katika Kombe la Shirikisho Afrika, Etoile du Sahel ya Tunisia wanatarajiwa kuwasili kesho kwa ndege maalum, tayari kwa mchezo huo wa Jumamosi.
    Yanga SC wanaikaribisha ESS katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    BIN ZUBEIRY inafahamu ESS watapanda ndege moja na ndugu zao, Esperance ya Tunis kwenda kwenye mechi za awali za michuano ya Afrika hatua hii. Esperance wanakwenda kucheza na El Marreikh nchini Sudan.
    Safari itaanza Alhamisi, yaani kesho na ndege itawateremsha kwanza Esperance nchini Sudan kabla ya kuja Dar es Salaam. 
    Na wakati wa kurudi pia, ndege itawapitia Esperance nchini Sudan ambao wanacheza El Merreikh Jumamosi pia.
    Mechi kati ya Yanga SC dhidi ya Etoile itakayoanza Saa 9:00 Alasiri inatarajiwa kuchezeshwa na marefa wa Msumbiji, ambao ni Samuel Chirindza atakayesaidiwa na Arsenio Chadreque Marengula na Celio de Jesus Mugabe washika vibendera.
    Jose Maria Rachide atakuwa mwamuzi wa akiba mezani, wakati Kamisaa ni Salah Ahmed Mohamed Saleh kutoka Sudan.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ETOILE WAJA KESHO DAR KWA NDEGE MAALUM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top